Mwanamuziki wa Taarab, Isha Mashauzi amewataka wanawake kupendana na kujaliana katika shida na raha bila kuchukiana.
Mashauzi amewahamasisha wanawake na mabinti wenye uwezo ili kuweza kuwasaidia watoto wa kike waliopo mashuleni waweze kupata pedi za kujistiri, kupitia kampeni ya ‘Namthamini’.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa wanawake siyo kama hawapendani bali muda mwingine wanakosa hamasa na namna nzuri ya kushirikishwa lakini anakiri wazi kuwa wanawake wanapendana na kusaidiana.
Pia Isha Mashauzi alitoa rai kwa watoto wa kike kuendelea kupendana na kujaliana ikiwa pamoja na kuthaminiana.
Mwanamuziki huyo ameachia nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Mwanamke Mpango Mzima’ iliyoanza kucheza jana katika vituo vya raido hapa nchini.