Mwanamuziki wa nyota wa Taarab nchini, Isha Mashauzi amesema kuwa muziki wa taarabu nchini hauwezi kufa kama baadhi ya watu wanavyodai kwani wao hawategemei kiki kama wasanii wengine.
Kauli hiyo ya Mashauzi inakuja baada ya kuwepo habari kwa wapenzi na mashabiki wakidai huenda muziki huo umekufa kwa maana hawasikii vijembe vya maneno wanavyopigana wasanii wenyewe kwa wenyewe kama wanavyofanya baadhi ya waimbaji wa muziki wa bongo fleva.
Mashauzi amesema kuwa Taarabu haiwezi kufa kwasababu muziki huo ukipigwa sehemu yeyote kila mtu ataujua fika kwamba hii ni taarabu tofauti na muziki mingine kwa hiyo hauwezi kufa.
Pamoja na hayo Isha ameendelea kwa kusema “naweza sema tu kwamba labda wanamuziki wa taarabu hawapendi zile kiki ambazo zipo kwa wanamuziki wengine, leo utasikia huyu sijui anatoka na fulani mara yule vile ndiyo mwisho wa siku aachie kazi yake mpya.
Mwanamuziki huyo ametambulisha nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Nebembeleze’ baada ya kukaa kimya kidogo kwenye muziki huyo toka mwaka jana.