Video vixen Bongo, Irene Hillary amefunguka na kusema kuwa hana mpango wa kuolewa na wanaume wa kibongo.
Video vixen amesema kuwa hawezi kuolewa na wanaume wa Bongo kwasababu wanaume waliowengi ni wababaishaji.
Irene alijizolea umaarufu siku za nyuma kutokana na kuonekana katika video ya kwetu iliyoimbwa na Rayvanny.
Pia umaarufu ulizidi baada ya kusemekana kutoka kimapenzi na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.
Irene alisema kuwa ameona wanaume wengi wa Kibongo wanapenda sana kuchezea wanawake hivyo haoni sababu ya kuutesa moyo wake kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mbongo.