Mugizaji wa Bongo Movies, Irene Uwoya amesema kuwa anajua watu wengi wanamchunguza kila kukicha kuhusiana na pesa zake na matanuzi anayoyafanya, lakini ukweli ni kwamba bado hawana majibu na kama wanayo ni ya uongo.
Kauli ya muigizaji huyo inakuja kufuatia hivi karibuni kufanya sherehe za gharama pamoja na kusafiri nje ya nchi huku kila mmoja akijiuliza anapata wapi pesa zote hizo.
Uwoya anasema kuwa, anaamini kuwa watu wengi hata usingizi hawapati, kisa tu, wanataka kujua ni wapi anapata pesa na yuko na nani kwa sasa, jambo ambalo anasema watapoteza muda mwingi na hawatapata majibu.
“Najua wazi kuwa watu hawafumbi macho, wananitafakari tu bila sababu za msingi na bado hawana majibu, lakini ukweli ni kwamba kupata majibu watachukua muda mrefu sana na watapoteza muda mno na hawatanijua, waendelee tu na kazi zao.