Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amefunguka na kusema kuwa anashangazwa na baadhi ya watu wanaosema mumewe Dogo Janja ni mdogo wakati mapenzi hayachaguai umri.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Uwoya kamfungukia mazito mumewe Dogo Janja ambapo amekiri kuwa anampenda mumewe na kusema anawashangaa watu ambao wanekazana kumsema ni mdogo kwani yeye anamuona mtu mwenye akili sana.
Ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya ilishangaza watu wengi ilipofungwa mwaka jana mpaka hivi sasa kuna watu ambao hawaamini kuwa wawili hao wameoana.
Na imekuwa ngumu kwa watu wengi kuzoea Mahusiano hayo hasa kwa sababu tofauti kubwa iliyopo baina yao kuanzia umri mpaka vitu vingine ambavyo vinaonekana baina yao.
Dogo Janja naye anaonekana amekolea na penzi la Irene kwani mara kwa mara anamposti mkewe na kumwagia sifa lukuki kama mke mwema na mwaminifu na kadhalika.