Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya ametangaza kuolewa tena kabla ya mwaka huu kuisha kwa sababu yupo kwenye mahusiano mazito.
Uwoya amefunguka hayo wakati akifungua duka lake la kuuza bidhaa za mabibi harusi kama vile magauni ya harusi, viatu na vitambaa.
Irene Uwoya amesema kuwa anatamani kuingia tena kwenye ndoa baada ya kufunga ndoa mbili za kwanza na sasa anataka kuingia kwenye ndoa nyingine.
Tayari Irene Uwoya ameshaolewa na aliyekuwa mume wake marehemu Hamad Ndikumana na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja.
Muigizaji huyo.