Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amewashukuru mashabiki wake baada ya kumpongeza mtoto wake Krish kupata kipaimara wiki iliyopita.
Krish Ndikumana; ni mtoto wa staa wa Bongo Movies na aliyekuwa msakata kabumbu wa kimataifa wa Rwanda, marehemu Hamad Ndikumana ambaye jana Jumapili Aprili 24, 2022 ilikuwa ni siku ya kipaimara ya mtoto huyo.
Hii ni baada ya komunio ya kwanza ambayo Krish aliipata mwaka jana katika Kanisa Katoliki jijini Dar es Salaam na jana ikawa ni kipaimara yake.
Uwoya anasema; “Namshukuru Mwenyezi Mungu, nina furaha iliyopitiliza kwa sababu haikuwa rahisi, namshukuru Mungu kwa kuniongoza na kunifunika kwa damu yake nikaweza kumlea mtoto.
“Pia nashukuru sana wazazi wangui ambao wana mchango mkubwa kwa mwanangu Krish. Pia nawashukuru walimu na wachungaji ambao wamemfanya mwanangu kufuata njia sahihi na kumjua Mwenyezi Mungu.”