Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya ameibuka na kudai kuwa pamoja na yote yaliyotokea lakini bado anampenda aliyekuwa mume Wake Msanii wa Bongo fleva Abdul Chende ‘Dogo Janja’.

Baada ya kufunga ndoa mwishoni mwa mwaka jana Irene na Dogo Janja walifikia tamati ya mahusiano yao mapema mwaka huu baada ya penzi Lao kugubikwa na wingu la usaliti wa kimapenzi.

Baada ya ndoa hiyo kuvunjika kumekuwa na maswali mengi ya tamati ya ndoa hiyo kwani hivi karibuni Uwoya amesikika akisema yeye hakubadilisha dini ili kufunga ndoa na Dogo Janja.

Irene Uwoya alipoulizwa endapo ameshapewa talaka yake na Dogo Janja Msanii huyo alijibu sijapewa talaka na Dogo Janja na sijawahi kuacha kumpenda hata siku moja, lakini maisha mengine lazima yaendelee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *