Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini, Irene Robert ameachia wimbo wa mpya ambao ameshirikiana na mwimbaji mwenzake, Christina Shusho.
Wimbo huo unajulikana kwa jina la ‘Sitalia’ ambao ameuachia wiki iliyopita kwenye mitandao ya kijamii mbalimbali ikiwemo you tube.
“Wimbo huu unamaudhui yakuijenga jamii katika kumwamini Mungu na kumwamini kuwa yeye anaweza kuwalinda dhidi ya maadui wote wanao wazunguka kwenye maisha yao.
Mbali na ujumbe huo mzuri lakini wimbo huo umeandaliwa katika mazingira mazuri yakuvutia na unaviwango bora kulingana na mahitaji ya soko la sasa.” alise,a Irene
Mbali na kolabo ya wimbo huu ‘sitalia’ mwimbaji Irene ana kolabo nyingine ambayo aliimba na mwimbaji wa Kenya, Guardian Angel ambaye anafanya vizuri nchini kwao na Afrika Mashariki, pia aliimba na mwimbaji Gaby kutoka nchini Kongo.
Mwimbaji huyo amejipanga vyema mwaka huu kwaajili kukuza zaidi mziki wake katika soko la ndani na nje ya nchini, kwani atafanya kolabo mbalimbali na wasanii wengine wakubwa wa hapa nchini na nje ya chini.
Irene aliyetamba na nyimbo kadhaa kama vile ‘Sidondoki, Niwewe , Tembea na mimi alisema lengo kubwa la kuimba ni kumtukuza Mungu na kuwafanya watu wamjue yeye kupitia uimbaji wake na ujumbe uliopo kwenye nyimbo hizo.
“Nawaomba mashabiki wazidi kunifatilia, kwani yajayo yanafurahisha, nitakuwa na mambo mengi ikiwemo kuandaa matamasha mbalimbali yakumtukuza Mungu na kutambulisha nyimbo.”
Mwimbaji huyo alianza uimbaji toka akiwa mdogo alipokuwa akiimba kwenye kwaya ya watoto, mbali na hapo mwimbaji huyo alianza uimbaji rasmi mwaka 2017.