Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Inspector Haroun amedai kwamba hakuwahi kuwa na bifu na Juma Nature bali bifu hiyo ilitengenezwa na mashabiki.

Inspector amesema kuwa wakati yeye anaoa mwanamke na kuhamia Kijitonyama kutoka Temeke ndio  kipindi ambacho Juma Nature na kundi lake la TMK walitoa ngoma ya ‘Shibe shibe’

”Katika mistari ya nyimbo hiyo wamesema ‘nyumbani ni nyumbani’ watu wakawa wanajua kuwa kuhama kwangu Temeke  ndio akanitungia nyimbo hiyo, baada ya muda kidogo mimi nimetoa ‘Mishe mishe’ basi ndio tukawachanganya sana kumbe  wala haikuwa hivyo mimi na Nature hatuna tatizo tuko pamoja sana”.

Msanii huyo amesema kufanikiwa kwake kulitokana na kushiriki katika  shindano la kusaka vipaji lililofanyika Don Bosco, ambapo DJ Bony Love alikuwa Jaji wa shindano hilo, yeye na Luteni Kalama  wakaibuka washindi.

Alipoulizwa  kuhusu wasanii kutoa nyimbo ambayo haidumu kwa muda mrefu, amesema inatokana na kukosa ubunifu ambapo wakati wao  wanang’aa walikuwa wanatumia muda mwingi kuandaa  ngoma zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *