Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro ametoa wito kwa wananchi wanaopenda michezo hasa mpira wa miguu kuipa ushirikiano timu ya Polisi ili iweze kufika mbele mpaka hatua ya Ligi Kuu.
IGP Sirro ametoa wito huo wakati akikabidhiwa vifaa vya michezo pamoja na hundi ya fedha ya shilingi milioni 20 na Mwenyekiti Kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa, Abbasi Tarimba. Makabidhiano yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Sirro amesema kuwa “Naahidi kwamba fedha hizi tutazitumia vizuri kujiandaa kwa ajili kupanda na kuingia Ligi Kuu kwa moto mkali na kuhakikisha kuwa tunaleta heshima kwa Jeshi la Polisi na wafadhili wetu mliotupatia vifaa vyetu leo niwaambie wenzangu ambao tutakutana kwenye Ligi Kuu tutapambana. Nitoe wito kwa wale wanaopenda michezo, jeshi lao la polisi, wale wanaopenda kuwa karibu na jeshi la polisi watupe ushirikiano ili nasi tuweze kufika katika LIigi Kuu”,.
Pamoja na hayo IGP Sirro ameendelea kwa kusema “SportPesa ni mdau mwelevu ameona umuhimu wa kuchangia fedha pamoja na kutoa vifaa vya michezo kwa ajili ya ku-support jeshi la polisi. Hii itatusaidia sana kwa sababu tukicheza sana michezo, maana yake tunakuwa karibu na jami, lakini siku zote tunafahamu wanaofanya michezo ni wachache ambao huwa wanajiingiza kwenye uhalifu”,.
Kwa upande mwingine, Tarimba amempongeza IGP Sirro kwa uwamuzi wake aliouchukua wa kupunguza timu za polisi na kuwa timu moja kwa sasa.
.