Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimetuma maombi Serikalini ilikupandishwa hadhi na kuwa Chuo Kikuu kutokana na kukidhi vigezo.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Dk Anthony Mavunde wakati akizindua Baraza la Tisa la Wafanyakazi la chuo hicho.
Waziri huyo ameahidi kufanyia kazi ombi hilo kwa kushirikiana na wadau wengine ili kufanikisha jambo hilo bila kupindisha utaratibu wa serikali.
Mavunde ametaka Baraza hilo jipya kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatekeleza mipango waliyojiwekea ambayo inaendana na utekelezaji wa wa mipango ya serikali.
Amesema mabaraza mengi ya wafanyakazi yanaykumbana na changamoto, ikiwemo ya kuikosa kuaminiana kati ya menejimenti na wafanyakazi hatua ambayo husababisha kila pendekezo linalowasilishwa kwenye baraza kukataliwa na wafanyazi.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Profesa Taadeo Sata alisema, chuo hicho kwa sasa kinatekeleza mradi wa upanuzi wa chuo hicho katika eneo la Msata, Bagamoyo mkoani Pwani.
Pia amesema pamoja na kwamba chuo hicho kinatafuta pesa kupitia vyanzo mbalimbali lakini kinahitaji msaada wa serikali ili kukamilisha ujenzi huo.