Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ibrah anatarajia kufanya show yake ya Home coming kwa mara ya kwanza ndani ya Mkoa wa Mtwara.

Ibraah anatarajiwa kutumbuiza mkoani humo mnamo November 27,2021 ndani ya uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Hii ni mara ya kwanza Ibraah kufanya show hiyo ambayo ameipa jina la CHINGA ambapo amewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi mkoani Mtwara.

Pia msanii huyo ameimwagia sifa albam ya Boss wake Harmonize anasema kwamba album ya Harmonize Haigh School ni kati ya album bora kuwahi kutokea Afrika.

Ibraah ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa mmoja kati ya wasanii wachache waliopata shavu la kusikika kwenye album hiyo inayotarajiwa kuachiwa November 5,2021.

Chinga ameandika “Kwangu Mimi Hii Ni Moja Ya Album Bora Kuwahi Kutokea Africa Na Am So Proud Kuwa Mmoja Ya Walioshirikishwa Humu Ndani!!.HIGH SCHOOL ALBUM OUT ON NOVEMBER Thank you TEACHER.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *