Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ibrah maarufu kama Chinga akubali mtoto anayeambia ni mwanawe baada ya mwanamke mmoja kudai kuwa amezaa na msanii huyo.
Kupitia akaunti yake ya Instagram Ibrah ameandika “Naam Ujio wa malaika huyu alie tukuka Duniani Licha ya MUNGU Kutimiza sifa Yake Kubwa Ya uumbaji pia Tunaziona Neema Pamoja na fadhiri Zake Kupitia Tabasamu Lilowekwa Katika Uso Wa Malaika Huyu Ambae Kila Mwenye Akili Timamu Angetamani Kuisikia Sauti Yake Ikiita Baba Au Pengine Mama.
Ameendelea kwa kuandika Taarifa Zimenifikia Kwasababu Mama Mzazi au Muhusika Mkuu Amenihusisha Na Amesema Yawezekana Mimi Ndio Mwenye Bahati Hii Ya Mtende Na Nimeona Nipost Hapa Ili Kuondoa Dhana na Maneno Yanayoendelea Mitandaoni Au ile Hofu Ya Kwamba Pengine Naweza Kuwa Mjinga Hadi ikafikia Kuitelekeza Damu Yangu.
Ibrah ameongeza kwa kuandika “Kitu Ambacho Hakiwezekani Na Hakitokuja Wezekana Ni wazi Kwamba Mama mtoto Alikuwa rafiki Yangu Siku Zanyuma Hilo Halina Siri Nandiomaana Sikusitushwa Sana Na Hizi Taarifa Kama Binadamu Wakawaida Nitafwata Taratibu Zote Kushirikiana na Uongozi Wangu Pamoja na Familia Yangu Kujihakikishia Kwamba Hii ni Kweli Damu Ya Mtwara Ili Taratibu Zingine Ziendele Itakuwa Faraja Kubwa Kwangu Pale VIPIMO vitakavyo Sema Yess Huyu Ni Chinga Maana Nitakuwa Nimeshapata Mwenzangu Wakushirikiana nae Katika Safari Hii Ya Kitendawili cha DUNIA. Mwisho amemalizia kwa kuandika “Nawaahidi tuu Hata Kama ikitokea Bahati Mbaya Vipimo vicatoa Majibu Tofauti Na tunayo Yatarajia Basi Still Nitakuwa rafiki Bora wa Malaika Mtukufu Ili Na Yeye Aonje Utamu Wa Dunia Bila Masemango Au Kubaguliwa Kwani Yeye Hahusiki & Hajuwi Chochote Zaidi Ya Kuzaliwa Na Anategemea Sisi Sote Tumfanye Mwenye Furaha THE KING OF NEW SCHOOL CHINGA”