Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila amemteua Bruno Tshibala kama Waziri Mkuu mpya katika Serikali ya kugawana madaraka.
Bwana Tshibala ataongoza taifa hilo hadi uchaguzi wa Urais unaotazamiwa kufanywa baadaye mwakani.
Alitimuliwa kutoka chama kikuu cha upinzani, UDPS, mwezi uliopita baada ya kupinga watu waliochaguliwa chamani kuchukua madaraka ya kiongozi aliyefariki Februari, Etienne Tshisekedi.
Waandishi wa habari wanasema kuwa kuchaguliwa kwa Bwana Tshibala kutawagawanya zaidi wapinzani wa Bwana Kabila baada ya mashauriano ya kujadili jinsi atakavyoondoka mamlakani kuporomoka juma lililopita.