Kesi inayomkabili mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ inatarajiwa kusikizwa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Mbeya.

Mbunge huyo ameiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi inayomkabili ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Mbali ya Sugu mshtakiwa mwingine ni katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika December 30, 2017, Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *