Klabu za Arsenal na Manchester United jana zimekamilisha uhamisho wa nyota wawili Alexis Sanchez akitua Man United na Henrick Mkhitaryan akitua Arsenal ambapo dau la Sanchez linakadiliwa kufikia £ 60m zaidi ya shilingi bilioni 164.

Zifuatazo ni rekodi mbalimbali za nyota hao wawili, Mkhitaryan mwenye miaka 29 raia wa Armenia na Sanchez mwenye miaka 29 raia wa Chile.

Katika msimu mmoja na nusu ambao Mkhitryan ameichezea Man United amefanikiwa kufunga mabao matano na kusaidia mengine sita huku Sanchez akifunga mabao 60 na kusaidia mengine 25 katika misimu mitatu na nusu aliyoicheza Arsenal.

Mkhitaryan amefunga mabao hayo matano katika michezo 39 ya EPL aliyoichezea Manchester United  huku Sanchez akifunga mabao 60 katika michezo 122 aliyoichezea Arsenal.

Mkhitaryan tangu ajiunge na Man United anashika nafasi ya 4 katika wachezaji waliopiga mashuti mengi yaliyolenga lango nyuma ya Jesse Lingard, Antony Martial na Juan Mata. Kwa upande wa Sanchez yeye anashika nafasi ya tano nyuma ya Olivier Giroud, Alex Iwobi, Alexandre Lacazette na Mesut Ozil.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *