Maprodyuza wa zamani ambao heshima zao zilikuwa kubwa ni Majani, Mako Chali na Master Jay.
Baada ya hapo wakaja mastaa wengine kwenye ulingo huo ambapo talents kama Lamar na Dunga.
Lakini baada ya miaka mingi kupita vipaji vingi vikaibuka ambapo mastaa wapya kama Nahreel na Mister T – Touch wakajikuta nao wanashika usukani wa Bongo Fleva ingwa Lamar amekuja na madongo dhidi yao na kudai watayarishaji wa muziki wa siku hizi wengi wanaringa na kujiona.
Lamar amelaumu kufanana kwa ngoma nyingi za mastaa wengi wa sasa wa Bongo Fleva kuwa kunasababishwa na maprodyuza wengi kujiona wanajua hivyo kushindwa kushauriana baina yao.
Ni kweli maprodyuza wa siku hizi wana ‘ego’?
Je, ngoma nyingi zinafanana?