Kocha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) Salum Mayanga amefanya mabadiliko kwenye kikosi kitakachoivaa Burundi kwenye mechi ya kirafiki leo uwanja wa Taifa.
Kikosi hicho kina mabadiliko kadhaa katika baadhi ya idara ikilinganishwa na kile kilichoanza kuivaa Botswana siku ya Jumamosi.
Golikipa Deogratius Munishi ‘Dida’ badala ya Aish Manula aliyeanza katika kikosi kilichopita huku katika nafasi ya ulinzi akiingia beki wa kati Salum Mbonde badala ya Erasto Nyoni .
Kiungo wa kati leo wataanza Himid Mao na Mzamiru Yasin ambapo Mzamiru anachukua nafasi ya Frank Domayo aliyenza katika kikosi kilichopita.
Viongo wa pembeni ni Farid Musa na Saimon Msuva, ambapo Farid amempumzisha Shiza Kichuya ambaye alionekana kutokuwa fiti katika mchezo uliopita.
Mwingine ambaye katika mchezo wa leo anaanza katika kikosi cha kwanza ni Salum Aboubakary, ambaye atakuwa msaidizi wa mshambuliaji pekee Ibrahim Ajibu.
Salum anachukua nafasi ya Ajibu huku Ajibu akichukua nafasi ya nahodha Mbwana Samatta katika kikosi kilichopita.