Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Heri Muziki amefunguka na kudai kuwa kama mpenzi wake Diva ameamua kuwa single hayo ni maamuzi yake mwenyewe hawezi kumuingilia.
Wawili hao walianza mahusiano yao mwaka Jana na kuuweka wazi kwenye mitandao ya kijamii.
Kauli hiyo ya Heri Muziki imekuja baada ya Diva kudai kuwa kwasasa yupo single kutokana na Heri Muziki kufichua ukweli kwa kusema kuwa wawili hao hawako kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa sasa.
Diva ambaye ni mtangazaji wa Clouds Fm amemtuhumu Heri kwa kumzalilisha baada ya kumkana redioni na baada ya hapo Diva aliingia Instagram na kusema kuwa yupo single akimaanisha ameachana na Heri Muziki.
Lakini pia Heri amefunguka na kudai kuwa wanachopishana na Diva ni kuanika mambo yao binafsi kwenye mitandao ya kijamii kwani tangu mwanzoni mwa mahusiano yao alimwambia hataki yawe public lakini aliendelea akaenda kuyaweka public.