Mwanamuziki wa R&B nchini, Heri Muziki amefunguka na kusema kuwa hawezi kurudiana tena na aliyekuwa mpenzi wake, mtangazaji Diva baada ya kuachana.

Heri amesema kuwa baada ya kuachana na Diva ndio mwisho wa yeye kuingia katika mahusiano na mtu maarufu kwani amejifunza mengi kutoka kwa Diva.

Amesema kuwa “Sikuwa nime-date na mtu maarufu before, wakwanza ni yeye, kwa hiyo baada yaku-date naye imekuwa ni experience kwangu, after that nisingependa ku-date na mtu maarufu.

Pia amefunguka na kusema kuwa  “Kurudiana na Diva siwezi, nafikiri hata yeye mwenyewe hawezi kurudiana na mimi, kwa hiyo tunaweza kumake peace hata kama hatutakuwa marafiki kila mtu anaendelea na maisha yake,”.

Wawili hao mara baada ya kupishana na kuamua kuachana kulipelekea Diva kutoa sauti ya Heri Muziki katika wimbo ‘Waambie’.

Credit Bongo5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *