Mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard atashiriki katika mechi dhidi ya Arsenal katika mzunguko wa kwanza ya nusu fainali ya kombe la Carabao leo baada ya kupona jereha.
Mchezaji mpya aliyesajiliwa kwa pauni milioni 15 kutoka Everton Ross Barkley hatoshiriki kwa kuwa bado anauguza jereha la nyuma ya goti.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ataendelea na adhabu ya kutokalia eneo la makocha uwanjani na badala yake kukaa katika viti vya mashabiki huku kikosi chake kikirudi baada ya kufungwa na klabu ya Nottinham Forest katika kombe la FA.
Granit Xhaka anauguza jeraha la kinena huku Shkodran Mustafi ambaye aligongwa akiwa hajulikani iwapo atashiriki.
Mfumo wa kiteknolojia wa video ya kumsaidia refa VAR utatumika katika awamu zote mbili za nusu fainali hiyo.
Arsenal haijashinda kombe hilo kwa kipindi cha miaka 25 huku Chelsea ikiweza kushinda mara ya mwisho 2015.