Aliyekuwa kiongozi wa Gambia, Yahya Jammeh ameondoka nchini humo kuelekea nchini Guinea baada ya kukubali kukabidhi madaraka kwa Adama Barrow aliyeshinda katika uchaguzi wa urais mwezi disemba mwaka jana.

Jammeh amesafiri kwa ndege kutoka Banjul hadi Guinea na baadaye kuendelea na safari yake kwenda Equatorial Guinea.

Kiongozi huyo jana alitangaza kwamba atang’atuka baada kuongozi Gambia kwa miaka 22 toka mwaka 1994.

Kwa mujibu wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi ECOWAS, Jammeh amewasili nchini Guinea .

Siku ya Alhamisi ECOWAS illituma vikosi vyake nchini Gambia kumshurutisha Bwana Jammeh kukubali Adama Barrow aapishwe.

Jumuiya hiyo inasema imesitisha oparesheni yake ya kijeshi Gambia lakini wanajeshi elfu saba watasalia nchini humo kudumisha usalama, huku Adama Barrow akitarajiwa kurejea Gambia kutoka nchi jirani ya Senegal muda mfupi ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *