Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmorapa ameachana na meneja wake Irene Sebuka baada ya wawili hao kuingia kwemye mgogoro wa kimaslai.
Sababu ya mgogoro huyo ni kwamba msanii huyo alipoanza kufanya show za mikoani hakukuwa na mrejesho wowote wa kumfaidisha meneja kitu ambacho pia kilimkwaza meneja huyo.
Pia Harmorapa wakati akienda mikoani kufanya show alikwa akisema kuwa show hazikwenda vizuri wakati meneja wake alishatumia zaidi yamilion 70 kwa ajili ya kumfanya Harmorapa kujilikana.
Meneja wa msanii huyo Irene Sabuka amesema kuwa anachojua yeye harmorapa alirubuniwa na promota bila kujali maslahi yake hiyvyo na yeye akaona isiwe tabu akaona bora kuachana nae.
Kwa upande wa Harmorapa amesema kuwa ni kweli amekuwa na matatizo ya hapo na hapo na meneja wake lakini haimaaishi kuwa hawafanyi kazi pamoja.
Harmorapa ni moja ya wasanii waliokuja kwa kasi sana katika tasnia ya muziki huku wakiata kiki na kujulikana na mashabiki kwa muda mfupi sana.