Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka na kusema kuwa mpaka sasa bado haamini kama anamiliki Kajala ambaye ni mwanamke anayependa kwenye chini ya jua hili.

Harmonize amefunguka na kusema kuwa ndiyo maana haachi kumshukuru Mungu kwa alichokifanya kwake.

Harmonize amesema kuwa, hakuna kitu kizuri kama kuwa na mwanamke ambaye unampenda kutoka ndani ya moyo wako ambaye akiishi na wewe unapata furaha ya ukweli na mambo yako yanakwenda vizuri.

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa, kwa upande wake amepata furaha ya kudumu ya maisha yake baada tu ya Kajala kukubali kuwa wake kwa mara ya pili baada ya kuwa pamoja mwaka jana na kuachana kisha kurudiana hivi karibuni.

 “Kuna wakati mtu huamini kabisa kinachotokea kwenye maisha yako, mimi siamini kabisa kama K (Kajala) ni wangu sasa. Amesema Harmonize

“Mwenyezi Mungu ni mwema sana, amenisogeza karibu kabisa na mwanamke wa maisha yangu, maana nitampenda siku zote, nampenda mno furaha ya maisha yangu ipo mikononi mwake sasa,” anasema Harmonize.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *