Mastaa wawili wa Bongo ambao ni wapenzi, Kajala ana Harmonize wameendelea kula bata sehemu mbali mbali huku wakiimarisha penzi lao.
Wawili hao wameonekana sehemu mbali mbali wakila bata kama vile wakiwa mbugani au na mahoteli makubwa sehemu mbali mbali.
Wapenzi hao wamenekana wakiwa hifadhi ya Taifa Manyara national park wakiwa wanakula maisha ambapo walikuwa wawili kwenye swimming pool pamoja na mpiga picha wao ambaye hajaonekana pichani.
Kajala kuna wakati alikuwa na kigauni cha uchokozi kabla hajabaki na kinguo maalum cha kuogelea ambacho kinaacha sehemu kubwa ya mwili wake wazi.
Baadhi ya maoni kwenye picha hizo ambazo Kajala kaziposti kwenye ukurasa wake wa Instagram, wapo waliompongeza lakini wengine wakiuliza kama wao hawajaguswa na makali ya tozo.