Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ametangaza kuwa kuanzia sasa tutegemee ngoma za kutosha kutoka kwa wasanii wa lebo hiyo kwani wamebaki wachache.
Kupitia ukurasa wa Mmoja ya wasanii wanaotoka ndani ya lebo hiyo Ibrah ameshare picha zake kisha Harmonize akashuka kwenye uwanja wa comment na kuandika kwamba kwa sasa wamebaki wachache hivyo ni ngoma juu ya ngoma.
Baada ya kimya cha muda mrefu Ibrah anaweza kuachia ngoma mpya kutoka kwenye kundi lao hilo la Konde Gang chini ya Harmonize.
Kauli ya wasanii hao imekuja baada ya wiki moja kuondoka kwa wasanii wawili wa lebo hiyo Chidy na Killy ambao kwasasa si wasanii wa lebo hiyo.