Mwanammuziki wa Bongo Flava, Harmonize anatarajiwa kutumbuiza katika kilele cha siku ya Mwananchini Agosti 30 mwaka huu katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Huu ni muendelezo wa matamasha ya klabu za mpira wa miguu nchini Tanzania, baada ya matamasha ya klabu mbili ambazo ni Simba na Azam kufanyika wikiendi hii.

Msanii Diamond Platnumz alitumbuiza kwenye tamasha la klabu ya Simba, ‘Simba Day’ Agosti 22 2020, huku Alikiba akiwa ndo mtoa Burudani Agosti 23 kwenye tamasha la klabu ya Azam, lililofanyika katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.

Kilele Cha Siku ya Mwananchi’ ni tamasha linaloandaliwa na klabu ya Yanga kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wapya, jezi mpya pamoja na kufanya matukio ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *