Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka na kuweka wazi Sakata lilimkuta siku chache zilizopita alipokuwa nchini Kenya.

Harmonize alifanya tamasha la Wasafi Festival Kenya tarehe 31 mwaka jana ambapo stejini aliwaambia Wakenya wanampenda kwa sababu Wakenya ni maskini wenzake ndiyo maana wanamuonesha mapenzi ya kweli katika muziki wake, lakini wao walitafsiri vibaya.

Harmonize alisisitiza hakuwa na maana mbaya ila kilichotokea kilikuwa ni lugha gongana tu na watu wa Kenya ila yupo nao sawa.

Unajua Kiswahili cha Wakenya na Watanzania ni tofauti ndiyo maana walitafsiri vile, ila mimi niliwaambia kwa nia nzuri tu kuwa watu wengi wananiuliza kwa nini Wakenya wanakusapoti sana kwenye muziki wako? Nikawaambia ni kwa sababu wao ni maskini kama mimi ghafla nashangaa watu wananishautia huku wanatikisa vichwa.

Huku wakisema usituite maskini maana tumelipa viingilio, sikutegemea kama itafikia hivyo, lakini nilitamani wajue kuwa sikumaanisha vibaya nawezaje kuwaita maskini wakati wao ndiyo wananiwezesha jamani”.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *