Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amejibu swali ambalo limekuwa likiulizwa na wengi hasa baada ya kushamiri kwa penzi lake na muigizaji Kajala Masanja baada ya kuachana na Sarah.
Harmonize alifunga ndoa ya halali na mrembo mwenye asili ya Italia Sarah na je vipi baada ya kuachana Talaka alitoa kwa mke wake huyo.
Harmonize amesema kuwa Sarah ni mtu ambaye amemeishi nae kwa miaka minne kama vijana kuna mengi wameyapitia kama changamoto anachoshukuru ni kila mmoja yupo kwenye maisha mengine sasa hivi na anamuombea Mungu amsaidie, talaka nimeandika.
Pia Harmonize amesema kuwa mwanzoni mwa huu mwaka nilikuwa nakamilisha Album nimefanya sana kazi so, nikahitaji kuwa na break na kuwapa nafasi watu wengine waachie kazi.
Vile vile ameongelea kuhusu masuala ya Ulinzi “Security is a lifestyle, lakini pia me naichukulia kama platform ya kusaidia vijana wenzangu, ukiangalia vijana wangu wote me nimefahamiana nao miaka kadha! So, naamini nikiwashika mkono nao wanaweza kusogea sehemu flani.”
Amesema “Mabaunsa wananisaidia sana, tunazunguka sehemu nyingi unaona kinachotokea, wanaokuja kunizunguka inawezekana 90% ni mashabiki lakini 10% wanaweza kuwa na nia ovu! Ao, Mabaunsa wanatusaidia sana sana.”.