Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amesema kuwa licha yeye kuwa shabiki wa Yanga hataki mashabiki wake wa muziki wajigawe kwa sababu anaishangilia timu hiyo.

Harmonize amesema mambo ya mpira yasichukuliwe kama mambo binafsi kwani mpira sio vita kwamba anashangilia Yanga basi mashabiki wake ndiyo wajigawe, pia ameahidi jinsi atakavyoshuka siku ya tukio hilo watu hawataamini.

“Mimi ni mwananchi timu yangu ninayoishabikia ni Yanga, kwenye michezo na hakuna hisia ngumu kwamba nikishangilia timu fulani eti mashabiki wangu wajigawe.

Harmonize ameongeza kwa kusema kuwa pia mpira sio vita, nia yetu ni kuusogeza mpira mbele wala sio uadui, ila ninachowaahidi siku ambayo nitashuka pale uwanja wa Mkapa hamtaamini”.

Pia Harmonize ametunga wimbo maalum kwa mashabiki wa Yanga kuelekea siku ya Wananchi ambayo itakuwa August 30.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *