Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize alipata nafasi ya kutembele Ofisi ya Baraza la Sanaa Taifa na kukutana na viongozi wa Baraza hilo.
Moja kati ya vitu ambavyo Harmonize amelishauri Baraza hilo ni pamoja na kuandaa matamasha ya Utamaduni na Michezo ili kukuza sekta hiyo ndani na nje ya Tanzania.
Basata wameandika “Rajab Abdul Kahali a.k.a Harmonize au Konde Boy ameiomba Serikali kuandaa Matamasha Mengi ya Sanaa na Utamaduni kama njia mojawapo ya kuwatangaza Wasanii wa nchi hii ndani na nje ya
Tanzania.
Hayo yalizungumzwa na Harmonize jana tarehe 7/12/2022 alipotembelea ofisi za BASATA jijini Dar
ES Salaam.
Aidha ameipongeza Serikali va awamu va sita chini Rais wetu mpendwa Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyowajali Wasanii hasa katika kuipambania Sanaa ili iweze kuwasadia kuinua maisha yao kiuchumi.
Pia amewashukuru BASATA chini va Katibu Mtendail wa BASATA Dkt.Kedmon Mapana kwa jinsi wanavyoweza kufanya kazi kwa ukaribu na Wasanii kupitia Mashirikisho na vyama vya Sanaa nchini katika kuendeleza Sanaa hasa katika kipindi hiki cha maendeleo ya Sayansi na Tekinolojia”.