Staa kutoka lebo ya WCB, Rajab Abdul maarufu ‘Harmonize’, amemtaja staa wa Marekani, Michael  Stevenson ‘Tyga’ kuwa ni mmoja wa wasanii wakubwa anaofikiria kufanya naye kazi mwaka huu.

Harmonize alisema tayari ameanza kufanya mazungumzo ya awali na Tyga ili kufikia makubaliano ya kuweza kufanya kazi pamoja.

Amesema kuwa “Wapo wasanii wengi, miongoni mwao nafikiria sana kufanya kazi na Tyga, mipango yetu ipo jikoni na wakati wowote mtapata mambo mazuri kutoka kwetu, huu ni mwaka wangu wa kuhakikisha natimiza sehemu ya ndoto zangu ili kuinua muziki wangu uwe wa kimataifa,”.

Kwa sasa staa huyo anafanya vyema na ngoma yake ya ‘Shulala’ akiwa kamshirikisha staa wa Nigeria, Korede Bello.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *