Baada miezi kadhaa kupita toka aachane na mpenzi wake Kajala Masanja staa wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize adokeza kuingia kwenye penzi jipya kwa mara nyingine tena.

Harmonize ameweka wazi hilo kwenye comment kupitia ukurasa wa DJ wake DJ Seven ambaye alikuwa anapiga muziki kwenye pool party iliyofanyika Arizona nchini Marekani.

Harmonize hakuwa mmoja kati ya wahudhuriaji kwenye party hiyo na ameandika sababu ya kuikosa party hiyo ilikuwa ni kubanwa na mpenzi wake. Harmonize ameandika “NINGEKUWA SINGLE ENZI ZANGU UNGE ENJOY JANA ….!!!! UKUBWA HUUUU MIE WAKULALA SAA 4 NABEMBELEZA.

Kwa tetesi zilizokuwa chini ya Carpet inasemekana kabla ya kwenda Marekani Harmonize alikuwa kwenye mahusiano ya siri na mrembo mmoja wa Kimarekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *