Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ameendelea kuonesha heshima kwa mwanamuziki mwenzake Alikiba kwa kumpongeza kwa kazi nzuri.
Kupitia kwenye moja ya postzake aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram(insta story) ameandika kama maneno yanayomtaka Alikiba kutumbuiza kwenye siku yake ya kumvalisha pete mpenzi wake.
Ameandika “Mtu amwambie mkongwe, mfalme Alikiba lazima aimbe kwenye usiku wa kumvisha pete mchumba wangu, huu muziki mzuri sana,” amesema Harmonize.
Harmonize ameandika maneno hayo huku akiambatanisha na kipande kidogo cha video akisikiliza wimbo ‘Utu’ wa msanii Alikiba.