Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize aomba kupumzishwa kusakamwa kwenye mitandao ya kijamii hii ni baada ya kuandikiwa walaka mrefu na Mtangazaji Mwijaku.

Mwijaku amemwandikia ujumbe Harmonize wakumtaka kutokuamini kwenye Falsafa ya kumlilia mwanamke kwa muda mrefu kwani mwanamke anayeitambua thamani ya muda wako ahitaji muda mrefu kumfuatilia.

Ujumbe wa Mwijaku uliunganishwa na picha mbili, picha ya kwanza ikiwa ni ya mrembo kutoka nchini Ethiopia na ya pili ni ya mrembo huyo akiwa na Harmonize kwenye gari. Mrembo huyo anaitwa Bezayittadesse ni mshindi wa Miss Africa Continent Ethiopia 2019/2020.

Ukaribu wa Harmonize na mrembo huyu wa Ethiopia ni wa muda mrefu toka Harmonize yupo kwenye ndoa yake na Sarah.

Picha linaendelea, mrembo huyo siku ya jana amepost picha akiwa kwenye gari na Harmonize bila kuweka neno lolote. Baada ya Harmonize kuiona post hiyo amepita kwenye ukurasa wa mrembo huyo na kuacha ujumbe huu ” Hii ni muda mrefu, acha kufanya hivi na kwanini unapost leo?”

Harmonize amekuwa na wakati mgumu kwenye mitandao ya kijamii juu ya kuweka wazi hatma yake na mpenzi wake Kajala ambaye inasemekana kuwa wameachana ikiwa ni muda mfupi tu toka amtambulishe kama mpenzi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *