Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka na kuthibitisha kuwa anamkubali sana mwanamuziki mwenzake, Alikiba kutokana na ubora wa kazi zake.

Hii ni baada ya kuonesha heshima kwa King Kiba na kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva.

Harmonize au Konde Boy amesambaza video yake fupi huku ukisikika wimbo mpya wa King Kiba wa Utu na kuambatanisha na ujumbe kwamba siku ya kumvisha pete mpenzi wake, lazima King Kiba atumbuize mashabiki wake.

“Mtu amwambie mkongwe, Mfalme Ali Kiba lazima aimbe kwenye usiku wa kumvisha pete mchumba wangu, huu muziki mzuri sana,” aliandika Harmonize ambaye ni C.E.O wa Konde Gang.

Hivi karibuni wasanii hao walionekana wakisafiri kwenye ndege pamoja wakitokea nchini Kenya wakirejea Bongo jambo ambalo liliteka mazungumzo mtandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *