Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ameachia wimbo mpya aliopa jina la Vibaya Kwenye wimbo huo Harmonize anaongea na aliyekuwa mpenzi wake Kajala ambaye ameachana nae kwa vita hivyo anamsihi watunziane siri licha ya kutengena kwao

Kuna mistari inapatika kwenye wimbo huo kama hii “Hata maadui zangu walikuwaga maadui zako hawawezi kukupenda wanakuvuta uwe kichekesho”.

Harmonize ameendelea kwa kuimba “Maana hata ukisambaza picha zangu za aibu ni sawa hata hunikomoi, Hata utupu wako ukitautandaza kwa watu wangu wa karibu hujengi hubomoi.

Harmonize hajaishia hapo ameendelea kumsihi Kajala kuwa amtunze mtoto wake kwani kuna kamchezo kabaya kanaendelea kwa mtoto wake.

Kwenye wimbo huo Harmonize ameimba maneno”Mama kuna kamchezo mtunze mtoto wako na watu wenye majungu, Nilikubali kuviacha vya dezo sababu ya mapenzi yako nikaachana na mzungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *