Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amemtambulisha rasmi mpenzi wake Briana raia wa Austalia kwa mashabiki zake.
Harmonize amepost picha za mrembo huyo kutokea nchini Australia na kuandika ujumbe huu “Nilikuwa nasubiri wasaha huu kumwambia kila mtu unamaana gani kwenye maisha yangu.
Nahitaji kukupenda, nakuahidi kuwa wako daima” aliandika msanii huyo ambaye kwasasa yupo nchini Marekani kwa shughuli za kikazi.
Baada ya ujumbe huo mrembo huyo alimjibu Harmonize kwa kuandika “Ninafuraha kuwa nawe kwenye maisha yangu”.