Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake wa siku nyingi msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja.
Tukio hilo limefanyika Juni 25, 2025 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam na kulipa jina la ‘Late Lunch’ huku likihudhuriwa na watu wa karibu wa wasanii hao ukiwemo uongozi wa lebo ya Konde Gang.
Harmonize amesema wamepitia mengi na msanii huyo na anashukuru hatua hiyo waliyofikia na mpenzi wake huyo.
Aidha amesema kwa wasiojua yeye na Kajala wamejuana zaidi ya miaka saba iliyopita tangu akiwa hana pa kulala mpaka kupata mafanikio aliyonayo leo.
Harmonize amesema kuwa yeye na Kajala wana historia ndefu kwani walijuana muda mrefu kwani toka wajuane wana jumla ya miaka saba.
“Mimi na Kajala tuna historia ndefu, tulijuana miaka saba iliyopita nililala kwake nikiwa sina pa kulala mpaka leo mnaponiona hapa,” amesema Harmonize
Kwa upade wake Kajala ammesema “Hakuna asiyejua tuliyoyapitia, pia mimi sio mkamilifu so nikaona kwa nini nisimsamehe, Harmonize nahaidi nitakupenda leo kesho hadi milele”. amesema Kajala
Mahusiano ya wawili hao yalijulikana rasmi Februari mwaka jana, lakini ilipofika Aprili penzi lao lilisambaratika baada ya kuvuja kwa picha chafu ambazo Harmonize ilielezwa alimtumia mtoto wa Kajala.
Takribani miezi miwili mwaka huu, Harmonize huko kwenye mitandao ya kijamii alionekana akililia kutaka kurudiana na mrembo huyo na mwisho wa siku wamekubali yaishe na kuvalishana pete