Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ameeleza sababu zilizosababisha yeye kuondoka katika Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya Diamond Platnumz.

“Nilimfuata Diamond nikamwambia tatizo ni nini mimi na wewe tunagombana? Akasema hivi: ‘Mimi nikimpa mtu heshima yangu, kama hatanirudishia naichukua kinguvu, unataka kushindana na mimi huniwezi kihela, huniwezi kiserikali, huniwezi kichawi nipe mkono tushindane’.

“Nikabaki nimezubaa, akaingia kwenye gari akaondoka. Siku iliyofuata nikaenda ofisini kwake kumuona.”

“Wakati Wasafi inaanzishwa mimi na yeye ndiyo tulikuwa tunapambania Wasafi, nilikuwa kimbelembele kusimamia vitu vingi, hata baadhi ya vifaa nilitoa mimi baada ya vya kwake kuchelewa.

“Kamati ilikuwa mimi yeye, Mustapha na mama Dangote, wakati huo hakukuwa na Babu Tale wala Sallam, wao walikuwa bize na Dizzim, kwa walikuwa hawaamini kwenye Wasafi Media.” amesema Harmonize.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *