Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kumuoa mpenzi wake Sarah.

Kwa muda mrefu kumekuwa na maneno mengi kuhusu Mahusiano ya Harmonize na Sarah huku wengi wakidai Harmonize hana mapenzi ya kweli kwa Sarah bali yuko naye kwa ajili ya pesa.

Harmonize ameweka wazi kuwa anampenda Sarah na hivi sasa yuko tayari kumuoa mwanamke wake huku akipuuzia maneno yote ambayo yanasemwa na watu.

Harmonize aliweka wazi mipango yake ya ndoa baada ya kukaa kwa muda mrefu kwenye uhusiano na mwanamke huyo.

Harmonize anafanya vizuri na nyimbo zake mbili ambazo ni Kwa ngwaru aliyomshirikisha Diamond Platnumz na wimbo wake mpya Dm Chick ambao amemshirikisha Sarkodie.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *