Mwanamuziki mkongwe wa Hip Hop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ni mmoja wa waasisi wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania tangu miaka ya 1990.

Sugu ni msanii wa kwanza kurekodi albam ya miondoko ya Hip Hop ya Kiswahili kwa gharama ya juu zaidi ndani ya Studio za MJ Records chini ya Master Jay.

Ni miongoni mwa waanzilishi wa awali kabisa wa Hip Hop Bongo akiwa na Da Young Mob ambao alishirikiana nao katika kinyang’anyiro cha Yo Rap Bonanza lililokuwa linaandaliwa na akina Kim The Boyz na Ibony Moalim katika miaka ya 1990, kabla ya kuwa rapa wa kujitegemea na kutoa albam yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Ni Mimi mwaka 1995.

Mbali na kuwa rapa, Sugu ni mwanaharakati wa haki za binadamu, mwanasiasa na mfanyabiashara.

Wakati ule, hoja ya Sugu ilikuwa; “Kuliko kuwa kimya bila kuwa active kimuziki nadhani sasa nalazimika kufikia mwisho na soon nitaweka rasmi mic chini.

Umri nao unasonga na majukumu mengine yanayohitaji muda wangu zaidi yanaendelea kuongezeka kwa neema zake Mungu.”

Mara ya mwisho, Sugu aliachia Albam ya Veto mwaka 2009, lakini alikuwa akitoa ngoma kadhaa mojamoja kama Freedom kabla ya kutangaza rasmi uamuzi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *