Kocha mkuu wa Yanga SC, Hans van der Pluijm amesaini mkataba mpya wa miaka miwili ili kuendelea kufundisha timu hiyo mpaka mwaka 2018.

Kocha huyo amesaini Mkataba huo makao makuu ya klabu hiyo maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaama baada ya kuiwezesha Yanga kutwaa mataji ya Ligi kuu na kombe la shirikisho la sakoTanzania “TFF”.

Pia kocha huo ameiwezesha yanga kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola.
Vile vile Hans Van der Pluijm ameiwezesha timu hiyo kucheza hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika na kutolewa na klabu ya Al Ahly ya nchini Misri.

Yanga inatarajia kucheza dhidi ya Medeama kwenye mechi ya marudiano ya kombe la Shirikisho Barani Afriaka, mechi hiyo itafanyika nchini Ghana Julai 27 mwaka huu

Hans Van Pluijm: Akiwa na akiwa na benchi lake la ufundi, kocha msaidizi Juma Mwambusi na kocha wa Makipa Juma Pondali.
Hans Van Pluijm: Akiwa na benchi lake la ufundi, kocha msaidizi Juma Mwambusi na kocha wa Makipa Juma Pondamali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *