Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameishukuru Serikali kwa kumteua kuwa miongoni mwa mabalozi wa kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari akibainisha kuwa atatumia nafasi hiyo ili lengo lifikiwe.

Leo Jumanne Juni 22, 2021 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba akiwa bungeni mjini Dodoma amemtangaza Mobetto, Mbwana Samatta, Edo Kumwembe na wengineo kuwa mabalozi wa kuhamasisha wananchi kulipa kodi.

Katika shukrani zake, Hamisa amesema ni heshima kuteuliwa kuitumikia nchi yake na ni mwendelezo wa Serikali ya awamu ya sita kuwaamini vijana katika utendaji kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *