Mwanamitindo Hamisa Mobetto amejibu sababu za kwa nini mzazi mwenzake Nassib Abdul ambaye ni msanii wa bongo fleva kutompost mtoto wao Dylan siku ya kuzaliwa kwake.
Mwanamitindo huyo amesema kuwa hajui sababu ya Diamond kutompost mtoto wao wakati ni siku yake ya kuzaliwa.
Aliongeza kwa kusema kuwa labda hilo swali aulizwe mwenyewe kwa nini hajampost mtoto wake katika siku ya sikukuu ya kuzaliwa kwake pia akasema kuwa baba yake mwenyewe hakuwahi kuwa na Akaunti ya Instagram hivyo hata yeye hakuwahi kupostiwa na haikuongezea wala kumpunguzia chochote.
Pia aliulizwa kama bado Diamond anatoa matunzo kwa mtoto wao lakini Mobetto hakutaka kuweka wazi suala hilo, ikumbukwe kuwa tu baada ya Diamond kutoshare kwa namna yoyote ile birthday ya mtoto wake siku ya Agosti 8, mwaka huu Hamisa Mobetto alimfuta kwenye Bio ya Instagram katika page ya Dylan.