Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu imezidi kuimarika na anatarajiwa kusafirishwa kwa matibabu ya awamu ya tatu siku za karibuni.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya mbunge huyo.

 Mbowe amesema kuwa mpaka sasa Tundu Lissu anaendelea vizuri na amefanyiwa upasuaji mara 17 toka alazwe hospitalini jijini Nairobi nchini Kenya.

“Tundu Lissu mpaka sasa amefanyiwa upasuaji mara 17 amewekewa damu nyingi kuliko mgonjwa yoyote katika hospitali ya Nairobi lakini Mungu ameendelea kutenda miujiza kwake, saizi mashine zote zilizokuwa zinamsaidia zimeondolewa, saizi hapumulii mashine tena, mirija yote aliyokuwa anatumia kwa ajili ya chakula imeondolewa na juzi kwa mara ya kwanza aliweza kukaa”.

“Matibabu ya awamu ya tatu ya Tundu Lissu yatafanyika nje ya nchi haitakuwa tena Kenya wala Tanzania, lakini kwa sababu za usalama hatuwezi kusema atakwenda sehemu gani au nchi gani, ukifika wakati sahihi tutasema hiyo awamu ya tatu ya matibabu itakuwa ya muda mrefu kidogo”.

Mbali na hilo Mbowe ameendelea kusema kuwa serikali inafahamu watu ambao wameshambulia Tundu Lissu na kudai wao hawana imani na vyombo vya dola nchini na kusema vyombo hivyo vimekuwa tawi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo hawana nia ya dhati katika kufanya uchunguzi juu ya sakata la Tundu Lissu kupigwa risasi mnamo Septemba 7, 2017.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *