Halmashauri nchini zimetakiwa kuweka mikakati madhubuti itakayosaidia kuwezesha walimu kutekeleza kwa umahiri mtaala uliofanyiwa maboresho pindi utakapoanza kutumika.
Wito huo umetolewa wakati wa kufungwa kwa mafunzo ya mtaala ulioboreshwa wa darasa la tatu na la nne unaozingatia vigezo katika kusoma kuandika na kuhesabu mkoani Kagera.
Akizungumza katika kilele cha Mafunzo hayo Mkurugenzi wa mafunzo ya mitaala kutoka Taasisi ya Elimu nchini, Finca Mwakabungu amesema lengo la kuanfda mafunzo hayo ni kutorudia makosa ya nyuma ambapo mitala iliyopelekwa mashuleni ilishindwa kutokana na walimu kutokuwa na ujuzi.
Halmashauri zimetakiwa kuto kukaa kando katika maandalizi ya matumizi ya maboresho ya mitalala ya elimu ili itakapofika wakati wa kutumika kwa mtaala huo walimu wote waweze kuwasilisha kwa umahiri na weledi kwa wanafunzi wao.