Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Hafsa Kazinja amefunguka na kusema kuwa amepitia kipindi kigumu ndani ya kipindi cha miaka 11 mpaka kupelekea kuokoka na kubadilisha dini.
Hafsa Kazinja ambaye alitamba na wimbo wake Pressure alichowahi kuimba akiwa na Banana Zorro amefunguka na kuelezea mapito aliyowahi kuyapitia kwa miaka 11 iliyopita ambapo anasema kuwa alikuwa katika wakati mgumu sana.
Pia mwanamuziki amesema kuwa amesema kuwa pamoja na ukaa kimya lakini kuna kilichomfanya kukaa kimya mabacho ni ugonjwa uliomsumbua kwa muda mrefu.
Hafsa amesema uwa uginjwa huo ulikuwa ukimtesa na kufikia hatua ya kunywa damu, na hata kuugua na kuteswa sana na majini hivyo hii ilimpelekea kuokoa na kumpokea yesu na kuachana na mambo ya kidunia.
Hafsa amesema kuwa yesu kwake ndio mponyaji, kwa sababu aliumwa sana na hata kufikia hatua ya kuuza nyumba, magari na kila alichokuwa nacho.
Hafsa anakiri kuteswa na majini hayo na kuamua kukoka na kuondoka katika uislamu kuingia katika ukiristo kutokana na matatizo hayo.