Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, H Baba amefunguka na kusema kuwa yupo tayari kutoa mahali na kumuona mwanamuziki mwenzake wa Bongo Fleva, Zuchu.
H Baba ameweka wazi ombi lake la kutaka kumuoa msani huyo pia yupo tayari kulipia mahari na kutuma wazazi wake waende wakaongee na wazazi wa Zuchu visiwani Zanzibar.

Kupitia akaunti yake ya Instagram H Baba amepost picha ya Zuchu na kushusha maneno yafuatayo “

Kama nitakubaliwa nikipata bahati hii nitakuwa tayari kumuoa @officialzuchu kama mtaniondolea vikwazo nimejipanga nipo tayari niambieni niandae Ng’ombe wangapi au nifanyeje”.

“Zuchu ni muislam mwenzangu lolote linaweza tokea, acha niandae wazee wangu wakisukuma wakamuone mama pia baba yake kule Zenji, ningependa nimuoe ni binti mstaarabu sana, acha nifate taratibu za kidini“.

H Baba alitamba enzi za nyuma na wimbo wake Mpenzi Bubu ambao ulimpa umaarufu na kumtambulisha katika soko la muziki wa Bongo Fleva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *